Maji safi kupatikana nchini kote mwaka ujao – Waziri mkuu

Anastase Murekezi na naibu mkuu wa masenata Bi Jeanne d’arc Gakuba
Waziri mkuu wakati alipokuwa kuwasilisha kazi ya serikali kuhusu namna inavyoendelea kushughulikia tatizo la maji safi, Anastase Murekezi aliambia wabunge kwamba mwaka wa 2017 maji safi atakuwa kupatikana akiptikana nchini kote.

Serikali ya Rwanda inalenga kuongeza upatikanaji wa maji safi nchini kwa asilimia 100 mwaka wa 2017 kutoka asilimia 74.2 ya mwaka wa 2010.

Ingawa ya waziri mkuu kuyasema hayo, uangalizi uliofanywa mwezi septemba ya mwaka jana na EICV4 ulionesha kuwa wanyarwanda wanaopata maji safi ni asilimia 84.8, waziri mkuu amesema kuwa hii ndio maana ya kulenga kutimiza asilimia mia moja mwishoni mwa mwaka ujao wa 2017.

‘’asilimia 100 ni lengo lisilobadilika, tunapaswa kuwa na mwendo kasi ili kufukia lengo hilo.’’ Waziri mkuu alisema.

Kwa kufikia lengo, waziri mkuu alisema kwamba wao watawekeza pesa nyingi katika viwanda vinavyotengeneza maji na kujenga mifumo mipya ya kusambaza maji katika maeneo mbalimbali.

‘’serikali inatekeleza miradi kadhaa ili kutatua tatizo la maji safi katika maeneo ya vijijini hasa wilaya za Nyagatare, Bugesera, Gatsibo, KayonzaRuhango, Nyanza, Gisagara, Nyaruguru, Rusizi, Rutsiro, Gakenke, Ngororero na Gicumbi zinazojulikana kukabiliwa na uhaba wa maji.’’ Waziri mkuu alitoa mfano.

Miongoni mwa miradi mikubwa serikali inajiandaa kukamilisha kabla ya mwaka 2016-2017 kumalizika ni kuongeza uwezo wa kiwanda cha nzove wa kuzalisha mita 40,000 za maji safi kila siku kutoka lita 25,000 kwa kila siku.

Serikali pia inajiandaa kujenga viwanda tatu vya kuzalisha maji wilaya za Nyagatare, Kayonza na Nyanza ambavyo vinatarajiwa kuzalisha lita 10,000 kila siku. Na serikali inajipanga kutoa mafunzo kwa makampuni binafsi ya kusaidia kuharakisha upatikanaji wa maji safi nchini .

Licha ya serikali kutumia nguvu nyingi kwa kutokomeza changamoto uhaba wa maji, wabunge walimkumbusha waziri mkuu kwamba bei ya maji inaendelea kuwa ghali.

Kuhusu tatizo hilo, waziri mkuu aliwaahidi wabunge serikali kuwa inapanga kuzungumza na mamlaka ya udhibiti wa huduma ili kupunguza bei ya maji safi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments