Vita vya ufafanuzi wa ukame na njaa kati ya Chama cha PS-Imberakuri na Wizara ya kilimo na ufugaji

Mukabunani Christine ambaye ni mkuu wa PS-Imberakuri na msemaji wa kongamano la vyama vya kisiasa chini Rwanda.
Siku zilizopita na mpaka sasa raia wa wilaya za Kayonza na Nyagatare mashariki mwa Rwanda walilalamika kufa na njaa iliyosababishwa na kiangazi ambacho hudumu siku nyingi.

Na baadhi ya raia walichagua kwenda Uganda kujitafutia chakula na wengine walishikwa mkono na serikali ambapo iliwasaidia kupata chakula.

Dkt Mukeshimana Geraldine ambaye ni waziri wa kilimo na ufugaji nchini Rwanda alisikika magazetini akisema kwamba tatizo liliyoko Nyagatare na Kayonza si njaa, yeye alibaini kwamba ni uhaba wa chakula uliyosababishwa na jua hatari.

Kwa mijubu wa ufafanuzi njaa ni uhaba wa chakula na ukame ni kiangazi kinachodumu siku nyingi.

Lakini Mukabunani Christine ambaye ni msemaji wa kongamano la vyama vya kisiasa nchini Rwanda na mkuu wa chama cha PS Imberakuri alisema yeye hakubaliani na waziri huyo. Akitoa hotuba yake wakati chama cha kiliberali walipokuwa kuadhimisha jubilei ya miaka 25 tangu PL kuanzishwa.

Bi huyo alisema kwamba yeye hakuelewi jinsi mahali paweza kukabiliwa na ukame kisha mtu akasema raia hawana njaa.

‘’kuna matatizo, kwa mfano ni njaa iliyopo nchini, nilimsikia waziri wa kilimo na fugaji akisema kuwa hakuna njaa nchini kuna ukame, sisi kama chama cha PS Imberakuri tunajiuliza tafauti iliyopo kati ya ukame na njaa, kuikweli njaa ipo nchini.’’

‘’ sijaskia kwa nini njaa ipo nchini, Rwanda haipaswi kukabiliwa na njaa, hii ni kosa la siasa mbovu ya kilimo kwa hiyo tunataka ibadilike, tuna mito, maji mengi hakuna sababu ya kukabiliwa na njaa.’’ Mukabunani alisema.

PS Imberakuri inasema kwamba kwanza , siasa ya kilimo inapaswa kubadilika ili kuwafundisha wakulima kumwagilia mashamba yao.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments