Airtel Rwanda yawashika mkono watu 500 wilayani Huye.

Mkuu wa Airtel Rwanda Bw. Michael Adjei Nii Boye akimpa raia mmoja kadi ya Mituelle de Sante
Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Rwanda imeshirikiana na raia wa Wilaya ya Huye kwa kufanya Umuganda na baada ya tukio hilo la kiraia Airtel iliwapa raia mia tano wa tarafa la Mukura, kusini mwa Rwanda makadi ya bima ya kiraia ‘’Mituell de sante’’

Huu umuganda ulishuhudiwa na katibu wa serikali katika wizara ya mamalaka ya ndani ambaye ni mjukumu wa maswala ya kijamii. Bi Alvera Mukabaramba alipongeza kampuni hii na alikumbusha raia kuwa kuungana nguvu katika hatua za kijamii ni chanzo cha maendeleo.

Dkt Mukabaramaba alishukuru AIRTEL kwa msaada wao wa kuwalipia bima raia wa Wilaya ya Huye.

“aacha niwashukuru Airtel kuhusu msaada wao wa kuwalipia raia wa Huye bima ya kiraia(Mutuelle de santé) na namshukuru kila mtu aliyepokea kadi hii na tuendelea kufanyia kazi pamoja kwa kuendeleze nchi yetu.’’
Mukabaramba alisema.

Mkuu wa Airtel Bw. Michel Adjei aliwashukuru raia wa kijiji cha Buvumu kwa kushrikiana na Airtel kufanya Umuganda kwa ajili ya kuendeleza nchi.

Na aliwahamasisha raia kutumia kadi hizo ili wawe na afya njema. Licha ya kushuhudia Umuganda, wao walitoa maua kwenye makaburi ya wahanga wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka wa 1994.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments