Sheria ya kuwaadhibu wateja wa wafanyabiashara wa mitaani inaweza kukataliwa

Shirika la kutetea haki za wateja nchini Rwanda ADECOR linasema kwamba wao wameanza kuchambua sheria iliyochapishwa katika gazeti la serikali.

sheria hii ni sheria iliyopendekezwa na mji wa Kigali ambapo sheria inasema kuwa mteja ambaye atakamatwa akinunua bidhaa mtaani, yeye na mfanyabiashara watalipa adhabu ya 10,000 Rwf na kuwapokonya bidhaa zao.

Lakini baadhi ya wanunuzi walilalamika kuwa serikali haipaswi kudhibu mteja labda kudhibu mfanyabiashara anayeuza katika maeneo kinyume na sheria.

Na hivi sasa, ADECOR inasema kwamba imeanza kuchambua kwa umakini sheria hiyo iwapo sheria kukiuka haki za wateja, ADECOR inaweza kuomba sheria kukataliwa.

Akiongea na makuruki.rw Theodoric ambaye ni mkuu wa shirika hilo, amesema kuwa mji ulianza kukimbiza wafanyabiashara wa mitaani mwanzoni na sasa ni mteja anayefuata kudhibiwa, hili ni tataizo la kujadili.

‘’ ni tangu zamani wakifukuza hawa wauzaji na kudhibu mteja ?, je hili ni suluhu ?’’ Theodoric amesema.

Kiongozi huyo aliendela kusema kwamba na wao walishangazwa na sheria hii na ndio maana wakishirikiana na wakili wao walianza kuchambua uamuzi huo baadaye na wao watatoa maoni yao.

Uzaburaho Theodoric aliongeza kwamba baada ya kuchambua hii sheria wakatambua kuwa inakiuka haki za mteja, wao wataomba mji wa Kigali kufuta pendekezo hilo.

‘’tukitambua sheria hii inakiuka haki za mteja, sisi tunawea kuomba kufuta hii sheria .’’

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments