Kaberuka au Sezibera huenda akachukua nafasi ya Dlamini Zuma.

Dkt Kaberuka (kushoto) na Dkt Richard Sezibera
Kuwa mweneyekiti wa tume ya umoja wa Afrika ni mojawapo wa cv kubwa katika maisha ya kila mtu barani Afrika na ni nafasi inayoheshimika barani kote.

Baada ya upigaji kura wa mtu aliyepaswa kujaza nafasi ya Bi. Dlamini Zuma kushindwa kufikia 2/3 vya wapigaji kura na upigaji kura kuahirishwa mwezi Januari mjini Addis ababa nchini Ethiopia,

tetesi zazuka, tetesi hizo zinasema kwamba huenda Rwanda kumchagu Dkt Donald Kaberuka ambaye alikuwa mkurugenzi wa Benki ya Afrika ya Maendeleo BAD au Dkt Richard Sezibera ambaye alikuwa katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC.

Fununu hizi zinasema kuwa baada ya upigaji kumalizika bila mshindi wa kuchukua nafasi ya Dk Dlamini Clarise Zuma, hii ni fursa ya kumchagua mtu ambaye atawakilisha Rwanda katika upigaji kura mjini Addis na huyu anaweza kuchaguliwa kati ya vinara wawili waliotajwa juu. Kwa mujibu wa tetesi kama ighe alivyoandika.

Gazeti la Daily nation limeandika kwamba Rwanda inataka kuchagua Dkt Kaberuka kama mgombea wake kwa kuonesha kwamba Rwanda ni nchi iliyoshinda mengi sana tangu miaka 22 baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi katika mwaka wa 1994.

Na katika mkutano huyo uliyofanyika mjini Kigali Rwanda tangu tarehe 10-18 mwezi Julai, viongozi waliamua kuwa huu ni muda Umoja wa Afrika kujijenga kiuchumi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments