Rwanda kupunguza bei ya viza.

Mamlaka ya uhamiaji nchini Rwanda imetangaza kupunguza bei ya viza ya kupitia kuhamia, kutembela na kuondoka Rwanda na hata viza ya utalii. Huku mamlaka hiyo inasema kwamba imebadili bei ya viza ikilinganisha na mabadiliko ya kubadilishana kwenye soko la kimataifa.

Viza ya utalii na ya familia ni dola za kimarekani 50, faranga za ulaya thamani 45 au ma pauni 35. Kama kawaida hii viza hupewa mtu anayehitaji kuzuru familia yake ambayo huishi Rwanda.

Kuhusu watu au kundi la watalii angalau wanne mpaka kumi ambao wanataka pasipoti ya utalii katika ukanda wa Afrika mashariki(EAC) hawa wanatarajia kulipa mia moja dola za kimarekani, pesa za ulaya 90 au pauni 70.

Na watu wanaotaka kuhudhuria mikutano hufanyika Rwanda, hawa wanatakiwa kulipa 30$, pauni 27 au euro 27 ingawaje bado ni bure kwa watu wanaotumia pasipoti za kidiplomasia.

Msemaji wa mamlaka ya uhamiaji Rwanda , Bw Yves Butera alisema kwamba haya mabadiliko yamesababishwa na mabadiliko ya faranga la waingereza kwenye soko la kimataifa. Na bei yakuingia au kuondoka nchini Rwanda kushuka kwa 20 kutoka 23 na bei ya viza ya Afrika mashariki ilipunguzwa kwa 35 kutoka 45 bei ya siku zilizopita.

Tangazo hilo linaserma kwamba huu uamuzi umeanza kutekelezwa tangu mwezi Julai,31, 2016 hadi kipindi cha miezi 12 kumalizika.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments