Angola waibuka kidedea FIBA Africa

Angola wakisherekea ubingwa
Na hivi sasa Jamhuri ya Angola ilioko kusini magharibi mwa Africa ndie nchi ya kwanza kwenye orodha ya mataifa machachari katika mchezo wa kikapu kiwango cha wachanga. Angola ilichukua ufalme baada ya kuicharaza Misri vikapu 86-82 kwenye mchezo wa fainali uwanjani ndogo wa taifa Amahoro mjini Kigali/Rwanda.

Hawa wachanga wa chini ya miaka 18 baada ya kusawazisha vikapu 76 kunako dakika za mchezo, wao waliongezwa dakika tano kisha Angola kuwachapa mabingwa mtetezi tofauti ya vikapu nne tu na baadaye nchi hiyo ilichukua ubingwa barani Afrika.

Hii ni orodha ya kama zilizoshika nafasi katika mashindano hayo ya mchezo wa kikapu barani Afrika kwenye kiwango cha wachanga
1. Angola

2. Misri
3. Mali
4. Tunisia
5. Rwanda
6. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
7. Algeria
8. Ivory Coast
9. Uganda
10. Gabon
11. Benin

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments