Chama cha Kiliberali : Donatile Mukabalisa achukua mikoba.

Mheshimiwa Donatile Mukabalisa ambaye ni spika wa bunge la Rwanda na hivi sasa ndiye aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha kiliberali PL, Bibi huyo amejaa nafasi iliyoachwa wazi na Protais Mitari baada ya kuiba pesa za chama na kutorokea katika nchi bado kujulikana.

Donatile Mukabaliosa alichaguliwa na kongamano la chama baada ya Mbunge Byabarumwanzi Francois kutokubali kuingia kinyang’anyiro.

Donatile alipigwa kura na wapigaji kura 569 kwenye 577 walioshuhudia uchaguzi na Munyangeyo Theogene alichaguliwa kuwa makamu Rais wa kwanza na wapigaji kura 472/577.

Donatile alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama baada ya kuchaguliwa kuwa makamu rais wa kwanza tarehe 16,machi,2014.

Chama cha kiliberali kilianzishwa katika mwaka 1991 baada ya Jvenal Habyarimana kushinikizwa kukubali siasa ya vyama vingi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments