Mugabe : ’Mtakiona’ Trump akishinda

Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaambia maseneta wa Marekani waliozuru taifa hilo kwamba watajutia kutofanya urafiki naye iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Maseneta hao Chris Coons na Adam Schiff waliambia gazeti la Politico nchini Marekani kwamba walikuwa katika taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji wa wanyama mwitu na kwamba waliomba kukutana na rais huyo na wakashangaa kwamba alikubali kuonana nao.

Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini Marekani inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa.

Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia : ’’Wakati Trump atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami’’.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments