Ingawaje mmemaliza masomo, maisha haendi kuwa rahisi. – Rais Kagame

Rais Paul Kagame amesema hayo wakati alipokuwa kukamilisha sherehe ya wahitimu 8,500 wa chuo kikuu cha Rwanda leo tarehe 29, Julai, 2016 uwanjani wa taifa Amahoro.

Katika hotuba yake Kagame aliwakumbusha kwamba wao wanaanza maisha magumu kuliko maisha ya chuo.

‘’mtu anaweza kujiambia kwamba baada ya kumaliza masomo yeye anaenda kula raha, hapana anajisikia uongo ! yeye anaenda kupambana kibarua na changamoto nyingi ambako atatakiwa kutumia nguvu zake zote.’’ Kagame alisema.

Rais wa Rwanda aliwaambia wahitimu kuwa wanaenda kugombana kwenye soko la kazi ambako watakutana na wapinzani wengi.

Kwenye soko la kazi si kila mtu kuajiriwa, idadi ya ajira inaweza ikawa ndogo kuliko watu wanaotaka kazi, hii ndio maana ya kupigania kazi na wa kwanza ndie ataajiriwa. ninawaambia hivi ili mjue kwamba nyinyi mnaenda kupitia changamoto nyingi kabla ya kutimiza ndoto zenu.’’
Rais Kagame aliongeza.

Hii ilikuwa mara ya kwanza Rais Paul Kagame kuongoza maadhimisho haya na hii ni mara ya kwanza wahitimu kusherehekea wakiwa pamoja baada ya miaka mitatu tangu chuo kikuu cha Rwanda kuumbwa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments