Wanafunzi waamini wa Islam wa vyuo wanatakiwa kupambana na ugaidi.

Wanafunzi 115 waamini wa dini ya Islam wanaosomea vyuo vikuu ndani na nje ya Rwanda katika mkutano wa siku moja kwenye makao makuu ya jeshi la Polisi ya Rwanda iliyoko Kacyiru na maafisa ya Polisi wametakiwa kuwa kwenye msitari wa kwanza kwa kupambana na itikadi ya ugaidi na msimamo mkali.

Katika hotuba yake, mkuu wa jeshi la Polisi IGP Emmanuel K. Gasana aliwaomba hawa wasomi kupata mwenendo wa uongozi wa taifa na alipata fursa ya kuwaomba kukomesha ugaidi na msimamo mkali.

‘’ushirikiano na umoja ndio njia sahihi ya kuepukana ugaidi na wenye msimamo mkali nchini kwetu. Ikiwa kujua lolote kuhusu kitu kinachoweza kuwa chanzo cha ugaidi julisha uongozi husika…hii ndio maana ya ushirikiano.’’ IGP Emmanul K. Gasana aliwaomba wanafunzi.

Mwakilishi wa hawa wasomi aitwaye Ishimwe Salim alisema wao waliapa kuwa watu wa kuigwa na kuzingatia mila na utamaduni wa Kinyarwanda na wao waliahidi kutumia mitandao ya kijamii kwa kuhubiri mipango kimaendeleo ya nchi.

‘’ tumeapa kuwa kwenye msitari wa kwanza kwa kupambana na ugaidi na kufafanua kiukweli Quran.’’ Salim alisema.

Mufti Habimana aliwaomba vijana hao kuwa wa kwanza kuzingatia mila na utamaduni wa Kinyarwanda, na aliendelea kusema kwamba itikadi ya msimamo mkali inaendelea kijitokeza katika waamini wa dini ya Islam baada ya mwaka jana waamini wa islam kukamatwa na kufungwa kutokana na uhalifu wa kigaidi.

Mkuu wa tawi la polisi ya Rwanda la kupambana na vitendo vya kigaidi Kamishna masaidizi wa Polisi Denis Basabose alisema madhumuni ya mkutano ilikuwa kushauriana ili kuchukua mikakati ya kupambana na uhalifu na kuhamasisha wanaufunzi wanaosomea nje ya Rwanda kutojiunga na watekelezaji wa vitendo vya kigaidi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments