Robert Mugabe ajibu baada ya kukosolewa

Vigogo wawili wa zamani katika vita vya uhuru nchini Zimbabwe, wakiwa pia washirika wa zamani wa karibu wa rais Robert Mugabe wamekamatwa Jumatano hii jioni.

Washirika hawa wa jadi wa rais Mugabe, ambao walimpelekea kufikia madaraka baada ya vita vya ukombozi katika miaka ya 1970, waliamua Alhamisi iliyopita kumkosoa mshirika wao huyo wa karibu, wakimtuhumu kwa utawala wake ni wa kidikteta.

Kukosolewa huko kunakuja kujiongeza katika hali mbaya ya kijamii na kiuchumi
pamoja na mlolongo wa maandamano yasiyokoma yanayoendeshwa na Mchungaji Mawarire. Wakati huo huo Rais Mugabe amejibu Jumatano hii usiku katika hotuba yake, ambayo iligubikwa na vitisho dhidi ya wale wote wanaotaka kumkosoa.

Hotuba hiyo ilidumu muda wa dakika arobaini na tano. Mugabe alimshambulia kwa maneno makali Mchungaji Mawarire, akisema kwamba hatovumilia ujinga wenye msingi wa kidini. "Sitovumilia ujinga uliyojengwa kwenye msingi wa kidini", Mugabe amemuonya mchungaji Mawarire ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Afrika Kusini.

Rais Robert Mugabe ameahidi kuwachukulia adhabu kali maveterani wa vita vya ukombozi, akielezea kwamba uchunguzi unaendelea kujua wahusika watangazo linalomkosa lililotolewa Alhamisi iliyopita.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments