"hakuna lolote la kuelezea wanyarwanda tena.’’ - Waziri Kanimba

Waziri wa biashara na viwanda Bw. Francois Kanimba anasema kwamba hawana sababu nyingine ya kuelezea wanyarwanda ya kutoanza ujenzi wa uwanja mpya wa maonyesho kwani wameshapewa ardhi na wao wanakaribia kuanza ujenzi siku chache zijazo.

Waziri Kanimba alisema hayo jana kwenye uwanja wa maonyesha Gikondo wakati alipokuwa kuzindua rasmi maonyesho kimataifa ya biashara kwa mara ya 19.

Mwaka uliyopita wa 2015, wakati waziri mkuu Anastase Murekezi alipokuwa kuzindua haya maonyesho, yeye aliambia wanahabari kwamba hiyo ilikuwa mara ya mwisho maonyesho kufanyika Gikondo na aliahidi kuwa mara ifuatayo maonyesho alipaswa kufanyika kwenye uwanja mpya wa Gahanga.

Waziri wa Biashara na viwanda akiuliza na wanahabari isipokuwa wao waliambia wanyarwanda uongo mwaka jana, Bw. Kanimba alijibu kuwa sabau kubwa iliyowafanya kuchelewa kujenga uwanja mpya wa maonyesho kule Gahanga/Kicukiro ilikuwa kukosa ardhi lakini alisema kuwa wao wako tayari kuanza ujenzi siku chache za usoni kwani wao wameshapewa ardhi.

‘’habari nzuri ya kusimulia wanyarwanda ni kwamba hivi sasa tumeshapewa ardhi na watekelezaji wanaendelea kutafuta kibali kwa haraka haraka, kabla ya kuanza ujenzi. Hakuna lolote lingine la kuelezea wanyarwanda tena.’’ Waziri Kanimba alisema.

Licha ya waziri Kanimba kusema hayo, ujenzi unaweza kuchelewa kwani katika hotuba yake yeye hakueleza wazi tarehe, mwezi na mwaka ujenzi kuanza zaidi ya kusema sisi tuko karibu kuanza ujenzi.

Maonyesho kimataifa ya biashara alianza tarehe 26,Julai,2016 na alivutia wafanyabiashara 419 na 271 ni wawekezaji wa ndani.


Waziri Kanimba akitembelea banda la kampuni inayoonyesha bidhaa za kiteknolojia

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments