Rusizi : Watu 11 wamekamatwa kwa tuhuma ya kuchimba dhahabu kinyume na sheria.

Wanaume 11 wametiwa nguvuni na jeshi la Polisi ya wilaya ya Rusizi kwa tuhuma ya kuchimba dhahabu kinyume na sheria kando ya mto wa Njambwe ulioko katika tarafa ya Gitambi. Magharibi mwa Rwanda.

Hawa watu ambao wanafungwa katika kituo cha polisi ni Mutuyimana Gaspard, Habimana Jean Pierre, Nyabyenda Bonaventure, Nsengumuremyi Gabriel, Bamporiki Eric, Ntibaziyaremye Enock, Ruticumugambi Boniface, Siborurema Dominique, Ntiyanyibagiwe Daniel, Bayibarire Felicien na Ntahombaye Selevate.

Mkuu wa Polisi wilayani humo Superintendent of Police (SP) Sano Nkeramugaba alieleza kwamba kuchimba migodi bila ruhusa ni chanzo cha kuharibu mazingira

“kuna njia halali ili mtu kuruhusiwa kuchimba migodi , na ukipita katika njia hizo unapewa kibali na ukahakikisha namna ya kujikingia ajali, hii ndio maana tunawaomba kujulisha polisi na uongozi kila ambaye mnamuona akifanya hivyo kinyume na sheria.’’ SP Sano alisema.

‘’ kazi ya kuchimba migodi si ambayo hufanywa na mtu yeyote, ni kazi ambayo kufanywa na watalaam, kufanywa na kila mtu huweza kusababisha watu kupoteza maisha.’’ Sp aliongeza.

Wakikatwa na hatia, wao watahukumiwa kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja jela na adahbu ya milioni sita mpaaka milioni kumi za Kinyarwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments