Rwanda kuwadhibu wafanyabiashara wa kitaani na wateja wao.

Baada ya mwaka mmoja na miezi miwili mji wa Kigali kupendekeza pendekezo la kuwadhibu wafanyabiashara wa kitaani na wateja wao, uamuzi umechapishwa katika gazeti la serikali la tarehe 18, Julai,2016.

Sheria hii inatarajia adhabu thmani 10,000 faranga za Kinyarwanda kwa yeyote ambaye atakamatwa akinunua na akiuzia bidhaa barabarani.

Mji wa Kigali unasema kwamba umependekeza uamuzi huo baada ya kuhangaikia idadi kubwa ya watu wanaotembea na bidahaa (nguo na viatu kwa uwingi) mitaani.

Hata hivyo, mji wa Kigali unawahamasisha wafanyabiashara hawa kujiunga na vyama vya ushiriki katika masoko ili wapewe mikopo (angalau 2,000,000) na waokolewe kodi katika kipindi cha mwaka mmoja tu.

Mji wa Kigali unasema kwamba kila wilaya ya mji inapaswa kujachagua ni nani ambaye anaruhusiwa kuhudumiwa kutokana na kuwa ni mwenye uraia wa Rwanda, mwenye kipato kidogo kutokana na mjibu wa viwango vya uchumi wa wanyarwanda na kukabali kufanyia biashara katika vyama vya ushirika.

Uongozi wa mji wa Kigali unasema kama sheria inavyosema, mtu ambaye atakatwa na hatia ya kuuzia na kununua bidhaa mitaani, atalipa adhabu ya 10,000 na kupokonywa bidhaa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments