Rwanda ni nchi ya kwanza kupambana matumizi mabaya ya bunduki katika ukanda.

Ripoti iliyotolewa kuhusu matumizi ya bunduki ndogo na nzito ilionesha kuwa Rwanda ni nchi ya kwanza kwa kupambana uhalifu uliotendwa na wahalifu wakitumia silaha ndogo au nzito.

Hii ni ripoti ilitolewa tarehe 25,Julai,2016 katika mkutano uliojumuisha nchi wanachama wa taasisi inayosimamia matumizi ya silaha ndogo RECSA mjini Kigali.
Mkutano huu ulilenga kuonesha kiwango cha uhalifu unaotendwa kwa hisani ya bunduki katika nchi ya Burundi, Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kenya, Uganda, na Rwanda.

Hii ripoti iitwayo Anlysis of Armed Crime Rate iliorodhesha Rwanda kwenye nafasi ya kwanza ya nchi ambazo zilikabiliwa na idadi ndogo ya uhalifu unao uhusiano na matumizi ya silaha katika ukanda wa Afrika mashariki.
Rwanda ilikabiliwa na uhalifu 421, Tanzania(9,646), Kenya (12,877), Burundi (26,041) na Uganda(34,512).

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Rwanda IGP Emmanuel K. Gasana alisema kwamba Rwanda iliweka mikakati imara ya kuzuia na kudhibiti usamabazaji wa silaha ndogo na nzito.

‘’ sisi tulisaidiwa na kuandika silaha katika mfumo wa kielektroniki na kutokana na huo mfumo tunamiliki orodha ya silaha hizo. Ndio maana tuliweza kupunguza matumizi mabaya ya silaha.’’ Gasana alisema.

Hii ripoti ilitengenezwa kati ya mwaka wa 2010 na mwezi februari,2016 kwa hisani kubwa ya benki ya kiafrika ya maendeleo BAD.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments