Watu 80 wauawa Afghanistan

Wizara ya afya ya Afghanistan imesema takriban watu themanini wameuawa na zaidi ya wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye mji mkuu Kabul.

Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili.
Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments