Meya wa zamani wa Gicumbi ametiwa nguvuni

Aliyekuwa meya wa wilaya ya Gicumbi kasikazini mwa Rwanda, Bw Mvuyekure Alexandre ameshikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo.

Makuruki.rw imefichuliwa kuwa Alexandre anashitakiwa matumizi mabaya ya milioni zaidi ya 33 katika pesa za Kinyarwanda.

Akiongea nasi, Msemaji wa Polisi kusini mwa Rwanda IP Gasasira Innocent amethibitisha kwamba Mvuyekure Alexandre amekamatwa jana alhamisi katika masaa ya jioni na hivi sasa Alexandre amepelekwa kituoni cha polisi ya Byumba.

IP Gasasira ametuambia kwamba Alexandre anatuhumiwa uhalifu wa matumizi mabaya ya fedha za VUP na kutumia hati bandia, makosa aliyotenda wakati alipokuwa madarakani ya katibu mtendaji wa tarafa ya Rubaya , wilayani humo.

‘’Alexandre ambaye alikuwa meya wa Gicumbi amefungwa korokoroni ya kituo cha polisi ya Byumba tangu jana jioni, yeye anashitakiwa makosa mawili yakiwemo matumizi kibinafsi ya fedha za serikali na kutumia nayaraka bandia.makosa aliyotenda wakati alipokuwa katibu mtendaji wa tarafa ya Rubaya katika mwaka wa 2010 kama ukaguzi wa mwezi jana ulivyoonesha.’’ IP Gasana alieleza.

Akipatikana na hatia , Mvuyekure anaweza kufungwa miaka tangu 7 hadi kumi na adhabu ya mara mbili ya pesa alizotumia kibinafsi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments