Sababu iliyofanya Rwanda kutokubali mapatano ya mahakama kimataifa ya kijinai - Rais Kagame atoa jibu.

Wakati yeye alipokuwa kuhitimisha elimu ya kiraia kwa mara ya tisa, Rais Paul Kagame alifafanulia wanakosi ambao walihudhuria ITORERO INDNGAMIRWA na wanyarwanda kwa ujumla kuwa sababu iliyofanya Rwanda kutosaini mkubaliano ya Roma, ni kuwa Rwana hakuoni uzito katika hii mahakama ya kimataifa.

Akijibu suala la mwanafunzi mmoja, Mheshimiwa Kagame alisema kuwa baadhi ya viongozi wa Afrika wanapenda kusaini mapatano mbalimbali, lakini baada ya siku chache wakaamua kufuta makubaliano. Kagame aliendelea kusema kwamba viongozi wa nchi za Afrika walikubali makubaliano ya Roma bali hivi sasa wao wanashitaki mahakama kulenga waafrika tu.

aliongeza kuwa ni haki zao kusaini mapatano ya Roma na pia ni haki yao kujiondoa wakati wao hawanufaiki kutoka mahakama hiyo.

Rais Kagame alisema kwamba Rwanda ilikataa kutia saini kwenye makubaliano kwani waliona kuwa mahakama hii hana mpango mzuri na wale waliosaini makubaliano wanajipanga kujiondoa kwani ICC haitoi sheria sawa kwa kila mtu.

“nimekusikia ukisema kuhusu ICC, sisi hatukusaini makubaliano ya ICC kwani hatukuoni uzito wa mahakama hiyo, wapo watu waliokubali ICC na hivi sasa wanalalamika kujiondoa, wapo watu waliokwama bila kunufaika ingawa wao hawajui lakini walikwama.’’ Kagame alieleza.

Rais Kagame alisema hivo, baada ya Louise Mushikiwabo ambaye ni waziri wa mashauri ya kigeni na ushirikiano na pia msemaji wa serikali ya Rwanda kutupilia mbali ombi la kumkamata Rais wa Sudan Bwana Omar Al-Bashir wakati alipokuwa nchini Rwanda kwa kuihudhuria mkutano mkuu wa umoja wa Afrika uliyofanyika huku Rwanda tangu tarehe 10-18, Julai mwaka huu.

Mahakama kimataifa ya kijinai alianzishwa katika mwaka wa 2002 lakini hivi sasa viongozi wengi wa Afrika wanashitaki ICC kulenga viongozi wa Afrika tu,

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments