Watu 9 washikiliwa na polisi Wilayani Ruhango na Nyagatare

Jeshi la polisi limeshika watu tisa wakiwemo viongozi wa ngazi za chini wilayani Nyagatare na Ruhango wakishtakiwa unyang’anyaji wa mali ya serikali zilizopangiwa wananchi ili kuwaokoa umaskini.

Hawa viongozi wanashitakiwa kutumia nyaraka bandia kwa kuiba pesa za VUP, wengi wao (watano) ni viongozi katika Wilaya ya Ruhango, kusini mwa Rwanda.

Katibu mtendaji wa tarafa ya Ntongwe na mganga wa mifugo ni baadhi ya waliotiwa nguvini na jeshi la polisi.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoani Kusini Chief Inspector of Police (CIP) André Hakizimana, alisema kuwa katibu mtendaji huyo anashitakiwa kutumia ripoti laghai kwa lengo la kunyang’anya wasiojiweza, mganga wa mifugo anashtakiwa kuwaomba wananchi pesa ili waandikwe kwenye orodha ya watu wanaopaswa kupewa ng’ombe katika Girinka.

Watu watatu wanatuhumiwa kuwaomba pesa wananchi wakiwaahidi kuwaandika kwenye orodha ya watu watakaopewa ng’ombe, katika unyang’anyi huo walipokea pesa za Rwanda milioni moja laki mia saba.

CIP Hakizimana alisema “Hawa waliotiwa nguvuni na polisi ndio wenye majukumu ya kuchunga, kupanga na kuweka matendoni mipango iliyotekelezwa na serikali lakini walifanya kinyume na sheri kwa lengo la kujinufaisha tunawaomba wanyarwanda wote kusimama imara na kupiga marufuku matendo haya na kupigania haki yao”.

Jeshi la polisi wilayani Nyagatare limetia nguvuni watu wanne wanaoshitakiwa kutumia nyaraka laghai na kunyang’anya pesa zilizopangiwa kuendeleza wasiojiweza katika VUP.

Msemaji wa jeshi la polisi katika jimbo ya mashariki Inspector of Police (IP) Emmanuel Kayigi alisema “Wanashitakiwa kushirikiana na viongozi wawili wa ngazi za chini. Viongozi hao walisaini katika nyaraka za ushirika laghai ndiyo sababu walipokea msaada wa VUP(vision Umurenge Program) thamani milioni mbili laki tano katika pesa za kinyarwanda.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments