Saini ya Diarra yazua sakata kati ya Rayon na AS Leopards.

Timu ya AS Leopards imetangaza kuwa iko tayari kumchukua mshambuliaji mkali wa timu ya Rayon Sports Ismaila Diarra mahakamani.
AS Leopards inalalamika kuwa Diarra amerasimshwa kuwa amesha saini mukubaliano mapya ya kuichezea Rayon baada ya kukubali kuichezea AS Leopard ya Kenya na kusaini mapatano.

Kiongozi wa AS Leopard ameambia tovuti ya goal.com kwamba wao hawawezi kukubali hivyo.

‘’tunahuzunika sana kuwa Diarra alikubali kuwa mchezaji wetu halafu akakubali kuichezea Rayon wakati yeye anajua hivyo ni kinyume na sheria. Sisi hatuwezi kukubali hivo. Hivi sasa tumesha chukulia kesi hiyo kwa wanasheria wetu ili kuipelekea FIFA.’’
Asava Kadima ambaye ni kiongozi wa As Leopard ametangaza.

Hata hivyo, Shirikisho la kandanda nchini Rwanda FERWAFA linasema kuwa haioni uzito katika malalamiko ya timu hiyo ya Kenya.

Mugabe Bony ambaye ni msemaji amesema kuwa FERWAFA imesimamisha kibali cha kwenda nchini humo kwani Diarra amesha panua muda wa kuichezea Rayon Sports.

Gakwaya Olivier anasema kuwa kabla ya timu yeyote kumsajili Diarra walipaswa kwanza kuuliza Rayon Sports kwani Diarra ni mchezaji wao.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments