Wakulima wito kuhudhuria kilimo cha umwagiliaji

Wito huo umetolewa na katibu wa serikali katika wizara ya kilimo na ufugaji Bw. Tony Nsanganira wakati alipokuwa akizundua kampeni ya kilimo cha umwagiliaji katika jimbo la Kasikazini mwa Rwanda, tarafani Butaro.

Tony alisema kilimo cha umwagiliaji inaweza kusaidia kupunguza athiri za mabadiliko ya anga na ukame wa muda mrefu yameathiri maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo, serikali imeanzisha mikakati tofauti tofauti ili kuhakikisha uzalishaji mzuri, matumizi bora ya ardhi, kutumia mbolea na kuchagua mbegu bora.

Akieleza sababu gani serikali ilichagua kuzindua hii kampeni katika kasikazini mwa Rwanda, Tony alisema kuwa ni kwa sababu ya kuongeza mazao ya viazi na kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji wakati wa kiangazi.

‘’mnahitaji kuhakikisha taaluma kwa kufanyia kazi katika vyama vya ushirika kwa ajili ya usalama wa vifaa hivi vya umwagiliaji. Nyinyi mnahitaji pia kushauriana na watalaam wa kilimo kuhusu namna ya kuweka utaratibu wa kutumia maji ili kuzalisha mazao yenye viwango vya kimataifa.’’ Tony aliwaomba wakulima.

Aime Bosenibamwe ambaye ni gavana wa jimbo la kasikazini aliomba wakulima kujadili na viongozi na watalaam wa kilimo ili wazalishe mazao yaani mboga na matunda sambamba katika ukanda na kuongeza mapato yao.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments