Majambazi wenye silaha washambulia Benki SACCO mjini Kigali.

Spt Hitayezu Emmanuel
Katika usiku wa tarehe 19,Julai, mjambazi wenye silaha za kienyeji wameshambulia benki UMURENGE SACCO ijulikanayo ‘’KIGALI SOLIDARITY VISION’’ katika tarafa la Kigali, Wilayani Nyarugenge, mjini Kigali ambapo hao majambazi waliua mlinzi na mwengine kujeruhiwa ingawa walishindwa kuiba pesa.

Msemaji wa jeshi la polisi mjini Kigali Spt Emmanuel Hitayezu aliambia sw.makuruki.rw kwamba takriban saa saba za usiku majambazi wenye silaha za kienyeji waliuawa mlinzi ambaye huitwa Nsengimana Kasiim na mwenzake Uwimana Jean Claude kujeruhiwa. Hivi sasa yule aliyejeruhiwa amepelekwa hospitalini ya CHUK.

Spt Hitayezu aliongeza kuwa ingawa ya mlinzi kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa, hao majambazi walishindwa kuiba pesa.

‘’ni majambazi wadogo, walijaribu kuangamiza jengo la benki lakini wao walishindwa kuvamia nyumba.’’ Msemaji alisema.

Washika doria walipofika baada ya washambulizi kuondoka na ni wao walioita polisi. Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hospitali ya Kacyiru.

Mpaka sasa hakuna mtu amesha kamatwa akituhumiwa shambulio hilo.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments