Afariki akipanda mlima Kilimanjaro

Gugu Zulu
Raia wa Afrika kusini Gugu Zulu amefariki dunia, wakati akijaribu kupanda mlima Kilimanjaro, nchini Tanzania.

Zulu mwenye umri wa miaka 38 na dereva wa mbio za magari alikuwa katika ziara ya kuchangisha fedha kuenzi juhudi za aliyekuwa Rais wa Afrika kusini Nelson Mandela, kuweza kuwasaidia pia wasichana kuweza kukidhi mahitaji yao maalumu.

Zulu na mkewe Letshego hawakuendelea na safari hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro, baada ya kugundua amepatwa na matatizo ya kupumua.

Awali katika mtandao wa Facebook, alielezea dalili za kusumbuliwa na mafua.

Ujumbe wa rambirambi umekuwa ukitolewa na watu mbalimbali na wengi wakimtakia kheri mjane wake, na binti yao wa mwaka mmoja. Lelethu.
Utaratibu wa kuurejesha mwili wa marehemu nchini mwake umekuwa ukifanyika.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments