AU SUMMIT2016 : Marais wanasemekana kujificha nyuma ya ghasia na ugaidi barani Afrika.

Bi. Francine Muyumba ambaye ni mkuu wa jukwaa la vijana barani Afrika
Kiongozi wa jukwaa la vijana barani Afrika Bi. Francine Muyumba aliambia wakuu wa nchi waliohudhuria mkutano mkuu wa umoja wa Afrika kwamba kama hawatakuweka mikakati imara ya kukomesha ukosefu wa ajira na tatizo la usalama, Afrika itaendelea kukabiliwa na mataitizo hayajakuisha.

‘’kama wakuu wa nchi za Afrika hawatakutatua tatizo la ukosefu wa ajira, Afrika itaendelea kuwa na matatizo, yaani vitendo vya kigaidi na uhaba wa usalama kwa ujumla.’’
Bi Muyumba alisema.

Akitoa maoni, Muyumba alisema kuwa Afrika inatakiwa kuanzisha mfuko maalum kwa vijana kwa ajili ya kuwasaidia kuwekeza.

‘’mfuko huo utasaidia vijana kuwekeza ili nao waweze kujikimu kimaisha, kuwekeza katika vijana ni kuwekeza katika Afrika ya siku zijazo.’’ Yeye aliongeza.

Kama vilivyotangazwa na umoja wa mataifa, vijana ndio wanaokumbwa na ukosefu wa kazi kuliko wengine kwani wao ni mara tatu zadi ya wanaokabiliwa na tatizo hilo.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments