Upigaji kura wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika umeahirishwa.

Leo hii ya jumatatu mwezi Julai, wakuu wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano mkuu wa umoja wa Afrika walitarajiwa kupiga kura mtu mwingine wa kujaza nafasi ambayo itaachwa wazi na Bi Nkosazana Dlamini Zuma baada ya kuondoka madarakani.

Lakini CCTV imetangaza kuwa wagombea wote hakuna mmoja wao aliyetimiza 2/3 vya wapigaji kura 53 .

Miongoni mwa wagombea watatu waliopigania nafasi hiyo ni Dr Pelonini Venson-Moitoi ambaye ni waziri wa mambo ya nje nchini Botswana, Dkt Specioza Niagaga Wandira Kazibwe aliyawahi kuwa makamu rais wa Uganda na Agapito Mba Mokuy ambaye ni waziri wa mashauri ya kigeni nchini Eqautorial Guinea.

Kwenye raundi ya kwanza, Specioza alipigwa kidole gumba na nchi 11, Bw Pelonini, nchi 16 na Agapito alipigwa kura na nchi 12.

Katika awamu ya pili, Specioza Kazibwe alitowa nje ya mbio ya mwenyekiti wa AU, Lakini Venson Moitio wa Botswana hakutimiza 2/3 vya wapigaji kura waliotakiwa kwa kuchukua mikoba kwani yeye alichaguliwa na nchi 23.

Upigaji kura wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika umeahirishwa mwaka ujao katika mkutano wa muungano huu wa umoja wa Afrika ambayo utafanyika mwezi Januari nchini Ethiopia kwenye makao makuu.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments