Watu wanne wamefungwa kutokana na uchimbaji kinyume na sheria

Wanaume wanne ambao ni raia wa Ngororero wamekamatwa na polisi ya kituo cha Kavumu wilyani humo.

Bazimaziki Fidele,36, Tuyishimire Noel,28, Ntibagawe mwenye umri wa miaka 55 na Tuyambaze Vincent wa miaka 19 wametiwa nguvuni na Polisi. Wao wanatuhumiwa kuchimba migodi ya aina ya Colta katika msitu wa serikali kijijini Tetero kinyume na vigezo na masharti ya kuchimba migodi.
Hawa wanaume walikamatwa tarehe 16, mwezi huu saba, saa kumi za jioni ambapo waliisha kuchimba kilo tano za hii migodi.

Mku wa jeshi la polisi wilayani humo, Senior Superintendent of Police (SSP) Marc Gasangwa aliwakumbusha raia kwamba kuchimba migodi katika njia hii ni kunyume na sheria na aliwahamasisha raia kutoa habari kuhusu uhalifu huo.

Alisema ‘’mtu anayetaka kufanya biashara ya uchimbaji, ni lazima kutafuta ruhusa la kuchimba , yeye anapaswa kuchimba kwa mijibu wa sheria ya kutetea mazingira na maisha ya wachimbaji.’’

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments