Polisi matapeli wawili walikamatwa na raia Nyamagabe.

Kwa ushirikiano na Raia wa Wilaya ya Nyamagabe, magharibi mwa Rwanda majuzi tarehe 4, mwezi Julai, mwaka wa 2016 walitia nguvuni watu wawili waliojifanya maafisa wa polisi.

Hawa polisi lagahi ni Nzihangana Alphonse ambaye hujiita Abdro mwenye umri wa miaka 31 na Nshimiyimna Simeon hujiita Japhet wa miaka 29.

Hawa wawili wanatuhumiwa ujanja ambapo wao walijiita maafisa wa Polisi kisha wakawaomba raia kuwatuma pesa kwenye simu ya mkononi ili kuwafungulia watu wao hufungiwa jela.

Kwa kawaida hawa wote ni raia wa tarafa la Bushekeri , Wilayani Nyamasheke ambao hawana lolote maarufu wanalofanya zaidi ya uhalifu wa uanganyifu.

Kama msemaji wa polisi katika jimbo la Magharibi mwa Rwanda, Chief Inspector Andre Hakizimana alivyosema, Yeye alisema kuwa hawa majambazi walikamatwa baada ya kituo cha polisi cha Gasaka kupokea milalamiko tangu mwezi Mei, raia walilamika kuwa wapo watu wanaojiita maafisa ya polisi ambao wanawaomba pesa kwa kuachilia uhuru watu wao lakini hawafanyi hivo.

CIP Hkizimana alisema ‘’baada ya kituo cha polisi kutambua namba zinazotumiwa na hawa majambazi, mmoja wa watu waliotakiwa kulipa pesa, kabla ya kukutana na hao watu uso kwa uso yeye alijiulisha polisi halafu yeye na polisi walikwenda mahali walipokubaliana kukutana na majambazi, kasha polisi iliwakamata baada ya majambazi kufika huko.’’

Licha ya kudanganya watu pesa, hawa wahalifu, watuhumiwa wanashitakiwa hatia ya kushughulikia watu ruhusa bandia ya kuendesha gari.

Afisa huyo wa polisi aliendelea kusema kwamba hawa watu walikamatwa baada ya kituo cha polisi kufikiwa na kesi 12 na majambazi kupokea faranga thamani 524,150 faranga za Kinyarwanda kupitia njia hiyo ya kijinai.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments