Soka : Nyigu wa Rwanda wameshuka chini kwenye viwango vya FIFA

AMAVUBI stars wa Rwanda wametetereka kwenye orodha inayotolewa kila mwezi na shirikisho la kandanda duniani FIFA. Hivi sasa nyigu wa Rwanda hukaa kwenye nafasi ya 111 wakati wao walikuwa kwenye nafasi ya 103 mwezi uliyopita.

Katika ukanda wa Afrika Mshariki, Uganda Cranes ya Uganda inaendelea kuongoza ambapo waganda wameshika nafasi ya 69, Kenya wa pili kwenye nafasi ya 86. na Jamhuri ya muungano wa Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 136 mwezi uliopita hadi nafasi ya 123 dunani.

Barani Afrika nchi ya Algeria imeendelea kuongoza huku ikiahika nafasi ya 32 duniani, Ivory Coast inashika nafasi ya 35 na Ghana ikiwa nafasi ya tatu na nafasi ya 36 duniani.

Kwa dunia, Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Ubelgiji na Colombia katika nafasi ya pili na tatu.

Orodha ya nchi zinazokuja mbele duniani kote kwenye orodha ya FIFA

Orodha ya nchi zilizoshika nafasi ya kichuja barani Afrika

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments