#AU SUMMIT : EAC hungoja kininja dhidi ya vita Sudan Kusini

Bi. Louise Mushikiwabo
Baada ya siku chache hali ya usalama kuzorota nchini Sudan Kusini kutokana na mapigano kati vikosi vinavyomuunga mkono Rais Salva Kiir na makamu rais wake Rieck Marchar mjini Juba, Jumuiya ya Afrika Mashariki inasema kuwa inaweza kutoa msaada kwa kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea kujitokeza nchini humo mwanachama wa EAC.

Waziri wa mashauri ya kigeni na ushirikiano wa Rwanda Bi. Louise Mushikiwabo anasema kwamba ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki na wao wanasikitishwa na vita inayoendelea Sudan Kusini kwa hivyo na wao watashughulikia pamoja suluhisho la mapigano katika huu mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika.

Yeye alisema ‘’ tunahuzunishwa sana na tatizo la kivita Sudan Kusini sisi kama bara la Afrika hususani katika ukanda ya Afrika Mashariki. Sudan Kusini ni nchi mwanachama mpya katika jumuiya yetu, sisi tunahofia, sisi kama, Rwanda walinda amani wetu walijeruhiwa katika mapigano siku zilizopita hii ndio maana tunafuatilia karibu tatizo hilo.’’

Waziri Mushikiwabo amesema kuwa mpaka sasa ukanda imeisha kuandaa kikosi cha ukanda ambacho kinachosubiri kutoa msaada wakati wowowte nchini Sudan Kusini (East African Standby Force).

Amesema ‘’tuliunda hii brigedi ili kutoa msaada dharura katika ukanda wetu, ni brigedi ya kutoa msaada dharura katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na pia tunafurahia kuwa ukanda wetu ni ukanda wa kwanza kujiandaa vizuri, brigedi iko tayari kutoa msaada siku chahce za usoni.’’

Amesema kuwa katika mkutano huu wa Umoja wa Afrika ambayo utahudhuriwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, wao watajadiliana tatizo hilo la Sudan Kusini, wakati wowote kupitisha uamuzi huyo, kikosi hicho kitachukua vikapo kwa kuelekea Sudan Kusini moja kwa moja.

Vita ilijitokeza tena nchini Sudan Kusini miezi miwili baada ya kuumba serikali ya umoja ambapo Riech Marchar ni makamu rais na Rais Salva Kiir ni rais wa Jamhuri hiyo.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments