Wizara ya elimu yatoa onyo wakurugenzi wanaoruhusu wanafunzi kwenda nyumbani bila mpango.

Katibu wa serikali katika wizara ya elimu anayejukumu maswala ya mashule ya msingi na sekondari Bw Olivier Rwamukwaya.

Katika taarifa iliotolewa na wizara ya elimu MINEDUC tarehe 13,Julai,2016, wizara hiyo inasema kuwa ni kinyume na sheria ya wizara ya elimu kuruhusu wanafunzi kwenda nyumbani kabla ya miezi mitatu kumalizika. Tangazo hilo linaeleza kuwa kila mkurugenzi anayefanya hivyo, Yeye anaweza kudhibiwa.

Olivier Rwamukwaya ambaye ni katibu wa serkali anayejukumu maswala ya mashule ya msingi na sekondari katika wizara hiyo amesema kwamba wakati wa kurudi nyumbani, wanafunzi wanatakiwa kuvaa sare za shule na pia aliwahamasisha viongozi wa elimu katika tarafa kushirikiana na wakurugenzi wa mashule kwa kushughulikia suala hilo.

Bw Rwamukawaya alisisitiza kuwa mkurugenzi ambaye huruhusu wanafunzi kurudi nyumbani kabla ya tarehe rasmi kufika ni kinyume na kalenda ya elimu na kuwa ni lazima kuacahana na tabia hiyo.

Je kalenda inasema nini ?

Tarehe 20, mwezi Julai,2016 : wanaofunzi wanaosomea kozi zao katika wailaya za Nyanza, Kamonyi,Muhanga na Huye, kusini mwa Rwanda na wilaya za Rusizi, Nyamasheke, Magharibi mwa Rwanda na wilaya za Nyarugenge, Kicukiro na Gasabo , mjni Kigali, wao wanaruhusiwa kwenda nyumbani mwao na tarehe tarehe ya kurudi darsani ni tarehe 5, mwezi Agosti, 2016.

Tarehe ya 21, Julai,2016 wanafunzi wanaopata masomo katika wilaya za Gisagara, Ruhango, Nyamagabe na Nyaruguru, Kusini mwa Rwanda na wilaya za Karongi, Rutsiro, Ngororero, Rubavu na Nyabihu magharibi mwa Rwanda nao wataruhusiwa kwenda katika likizo na tarehe ya kurudi katika masomo ni tarehe 6, mwezi Agosti, 2016.

Traehe 22, Julai, wanafunzi wa jimbo la mashariki na kusini na wao watarudi kwao na tarehe ya kuanza masomo ni tarehe 07, mwezi wa nane mwaka huu.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments