Waziri Mushikiwabo amefunguka baada ya kifo cha mbunge nchini Burundi.

Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Rwanda Bi. Louse Mushikiwabo amesema kwamba Yeye amehuzunishwa sana na kifo cha Bi Hafsa Mossi ambaye amekuwa mbunge aliyewakilisha nchi ya Burundi katika bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA)

akitumia ukurasa wake wa Twitter Bi Mushikiwabo amesema kuwa marehemu huyo alikuwa rafiki yake.

Alisema ‘’ nimesikitishwa na kupoteza mtu wangu Burundi, Hafsa Mossi aliwahi kuwa mwanamke mzuri, RIP dada.’’

Hafsa Mossi aliuawa leo akipigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments