#AUSUMMIT2016 : Hatutakubali uongozi ambayo hukiuka haki za kibinadamu - Dlamini Zuma

Kiongozi mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini Zuma amesema kuwa Afrika kama bara kwa ujumla ni lazima iwe na uongozi ambayo huheshima haki za kibinadamu.

Zuma alisema hayo hii leo tarehe 13,Julai,2016 wakati alipokuwa kufungua rasmi mkutano mkuu wa umoja wa Afrika kwa mara ya 27 mjini Kigali/Rwanda.

Alisema ‘’ ni kitu muhimu kuzindua mkutano wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe huendelea kujitokeza Sudan kusini baada ya miaka miwili ya mazungumzo na miezi miwili baada ya uumbaji wa serikali ya umoja lakini licha ya wananchi kusherehekea miaka mitano ya uhuru, wao wanaendelea kufa katika mapigano, sote kama waafrika huu ni muda wa kutokubali uongozi hunyanyasa raia.’’

“serikali na uongozi halali ni uongozi hulinda mwananchi mdogo na wale wa juu sio uongozi wa kuuuwa wananchi vile vinavyotokea Sudan kusini ni kinyume na sheria, Afrika haitaendelea kukondolea macho mauaji katika Sudan kusini na mahali popote barani Afrika.’’
Bi. Nkosazana aliongeza.

Mkutano huyo huendelea kufanyika wakati nchi nyingi za Afrika hususani Sudan kusini zinaendelea kukumbwa na machafuko ya kivita ambapo wananchi wanaendelea kuuawa kikatili. Ingawa Bi. Zuma anasema kwamba Afrika itaendelea kulinda amani nchini humo.

Kama mada ya mkutano inavyosema, Dkt Nkosazana Dlamini-Zuma amesema kwamba Afrika itaendelea kufanya chochote kinachowezekana kwa kutetea haki za mwanamke na haki za kibinadamu kwa ujumla.

Mwishoni mwa mkutano huu, wakuu wa nchi za Afrika ambao watahudhuria mkutano huo wanatarajia kuijadili matatizo mbalimbali yakiwemo na tatizo la usalama.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments