Ngoma : Katibu mtendaji amekamatwa wakati alipokuwa kuangusha bendera.

Katibu mtendaji wa kijiji cha Gituza, katika tarafa la Rukumberi, Wilayani Ngoma mashariki mwa Rwanda ametiwa nguvuni na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kukamatwa wakati alipokuwa kuangusha bendera la nchi ya Rwanda.

Habiyaremye Joseph ambaye ni katibu mtendaji wa Gituza amekamatwa usiku wa manane ya tarehe 12, Julai, mwaka wa 2016.

Msemaji wa polisi Inspekta wa Polisi Emmanuel Kayigi aliambia sw.makuruki.rw kwamba habari hiyo ni ya ukweli.

Alisema ‘’ndiyo !, Joseph amesha kamatwa lakini uchunguzi bado kuendelea ili kujua sababu iliyomfanya kuangusha bendera la Nchi.’’

IP Kayigi aliongeza kusema kwamba katibu huyo ameambia polisi kuwa alifanya hivyo kwa kujaribu kama washika doria walikuwa kusubiri.

Habiyaremye Joseph amekamatwa na washika doria kisha kupelekwa mikononi mwa polisi karibu nao huko Ngoma, Msemaji wa polisi amesema kuwa mtuhumiwa amefungiwa katika kituo cha polisi ya Sake.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments