Kizza Besigye aachiliwa uhuru kwa dhamana Uganda

Besigye ametakiwa kuwa akifika kortini kila baada ya wiki mbili
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye, ambaye amezuiliwa kwa wiki kadha, amepewa dhamana na Mahakama Kuu nchini humo.

Jaji Wilson Masalu Musene amempa kiongozi huyo wa chama cha Forum for Democratic Change dhamana ya dola 30,000 za Marekani.

Jaji amemwamuru Dkt Besigye kutojihusisha na vitendo vya kuzua ghasia na adumishe amani katika jamii hadi kesi ya uhaini inayomkabili isikizwe na uamuzi kutolewa.
Ametakiwa awe akifika kortini mara moja kila wiki mbili kuanzia Julai 26.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wafuasi wa Beisgye wameimba wimbo wa taifa wa Uganda na kushangilia baada ya kiongozi wao kupewa dhamana.

Besigye amerejeshwa seli kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kumwachilia huru kwa dhamana hiyo.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments