Dkt Binagwaho amefunguka baada ya kufutwa kazini

Bi. Dkt Agnes Binagwaho
Baada ya Bi. Binagwaho Agnes kutimuliwa kwenye uongozi wa wizara ya afya, jana usiku, akitumia ukurasa wake wa Twitter Binagwaho ameshukuru Rais Paul Kagame kuwa alimpa nafasi ya kuongoza wizara kubwa kama wizara ya afya.

Alisema kuwa ni kitu cha kujivunia kutumikia majukumu kama hayo chini ya uongozi wa Rais Paul Kagame.

Yeye alisema ‘’ ni heshima yangu kubwa kuwahi Rwanda chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Paul Kgame, nilijifunza mengi na mimi ninajivunia kuwa nimekuwa kufanya kazi katika wizara ya afya.’’

Dkt Agnes Binagwaho aliwahi wizara ya afya tangu mwaka wa2011 baada ya kutumikia majukumu ya afya katika viwango mbalimbali.

Janvier Karangwa

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments