#AUSUMMIT2016 : Dlamini Zuma ameomba waafrika kijijenga

Akizindua mkutano mkuu wa umoja wa Afrika ambao unafanyika kwa mjini Kigali kwa mara ya 27, Bi Dkt Dlamini Nkosazana Zuma ambaye ni mkuu wa tume ya umoja wa Afrika ameambia washiriki kwamba Waafrika wanapaswa kufanya iwezekanavyo ili wajijenge kiusalama.

Dlamini Zuma amesema ‘’ ili sisi tutimize ndoto zetu, ni lazima kushirikiana kwa kujishughulikia amani kupitia ushirikiano na umoja wetu, hii ni njia halali ya uhuru, uamuzi wa marais wetu ya kuunga mkono na kushirikiana na umoja wa Afrika katika shughuli za amani itakuwa msingi halisi ya kujikomboa.’’

Amekumbusha watu ambao wameshiriki mkutano huyu kwamba ni jukumu lao kutetea haki za mwanamke, msichana na haki za kibinadamu kwa ujumla.
Mkutano huu wa AU umeanza leo hii ya tarehe ya 10 mwezi Julai hadi tarehe 18, Julai, 2016.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments