Polisi waua mtu mwengine mweusi Marekani

Polisi waua mtu mwengine mweusi Marekani
Mtu mwengine mweusi amepigwa risasi na kuuawa mapema leo na polisi wa trafiki katika jimbo la Minnesota Marekani.

Dereva huyo ambaye alikuwa amembeba mpenzi wake ndani ya gari lao alisimamishwa na polisi katika eneo la Falcon Heights kisa , taa moja ya upande wa nyuma wa gari lake ilikuwa imepasuka.

Alipoulizwa leseni yake akanyosha mkonowe kana kwamba anaichukuwa upande wa nyuma na polisi huyo akampiga risasi 4 papo hapo.

Mpenziwe Lavisha Reynolds, na mwanawe walikuwa naye ndani ya gari hilo.

Bi Lavisha Reynolds, alikuwa akipeperusha moja kwa moja tukio hilo kupitia kwenye mtandao wa Facebook.

Japo mkanda huo umefutwa kwenye Facebook ,watu wamejitolea kuuchapisha tena na tena.

Mkanda huo unamuonesha Philando Castile akivuta pumzi yake ya mwisho huku afisa huo akiwa amesimama wima kila mara akimtishia bi Reynolds asidhubutu kusongeza mikono yake la sivyo atampiga risasi.

Mwishowe bi Reynolds anakamatwa yeye na mwanawe wanahamishwa hadi kituo cha polisi.

Video inaonyesha Philando Castile akifuja damu ktoka kifuani huku polisi mwenye hasira akiwa bado anamuelekezea Bunduki.

Bw Castile, 32, alikuwa msimamizi katika hoteli moja inayowaandalia watoto wa shule ya Montessori vyakula.

Mpenziwe anasema alikuwa na idhini ya kubeba silaha halali.

Kisa hicho kinatokea huku kiandamana baada ya mauwaji mengine ya mtu mweusi mjini Lousiana.

Mauaji ya Alton Sterling, yameibua hasira miongoni mwa wenyeji wa mji huo wa Baton Rouge ambapo Sterling alikuwa akiuza CD.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments