Niqab ni marufuku nchini Rwanda.

Mtindo wa Niqad, ni nguo amabazo hutumiwa na wanawake waumini wa kislamu ambako wanajificha sehemu zote za mwili mpaka usoni.

Mufti mpya wa dini ya Kislamu Sheikh Hatimana Salim amesema kwamba wameamua kupiga marufuku mavazi ya Niqab kwani wako watu wanaovaa Niqab kwa kuvuruga usalama, kwa hivyo ni kwa lengo la kujikingia uhalifu.

Katika hotuba yake asubuhi ya leo katika sherehe za kutimiza mwezi Ramadhan, alisema kwamba uamuzi huo ni muhimu.

Alisema ‘’wakati mtu amejikificha uso wake, mara nyingi ni vigumu kutambua ni nani…., wapo watu wanaotumia Niqab kwa kutenda uhalifu’’.

Shekh Salim Hitimana
Sheikh Salim Hitimana amethibitisha kuwa Niqab haitakubaliwa nchini Rwanda

Baadhi ya wanawake walioongea na gazeti la Izubarirashe walisema kwamba waliaambiwa kwamba hawatakubaliwa kuvaaa Niqab.

Niqab inatumiwa sana katika nchi za Kiarabu na nchi za kiisalamu kama Saudi Arabia,Yemen, Oman na United Arab Emirates Somalia, Syria, Afghanistan, Pakistan, India, Bangladesh, Palestine.


Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments