Oscar Pistorius afungwa jela miaka sita

Pistorius alimuua mpenzi wake Februari 2013

Bingwa wa mbio za Olimpiki za walemavu Oscar Pistorius, kutoka Afrika Kusini, amehukumiwa kufungwa jela miaka sita kwa kumuua mpenzi wake mwaka 2013.
Alikuwa amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela zaidi ya miaka 15.

Mawakili wa upande wa mashtaka na wa upande wa mshtakiwa wanaweza kukata rufaa.
Uamuzi wa mahakama nchini umetolewa baada ya kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia kuwa mauaji mwezi Desemba baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa.

Pistorius, 29, alimpiga risasi Reeva Steenkamp mara nne February 2013. Amepelekwa jela ya Khosi Mampuru mjini Pretoria.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments