Waziri mkuu awaomba wafanyakazi wa kilimo na ufugaji kuachana na unyang’anyi

Wakati wakutimiza jando ’’ITORERO’’ la wafanyakazi wanaoshughulikia taaluma ya kilimo na ufugaji lililofanyika Wilayani Huye, kusini mwa Rwanda tarehe 5 Julai 2016, waziri mkuu nchini Rwanda Anastase Murekezi aliwaomba washiriki kuwa waaminifu katika kazi yao ya kila siku.

Akiwakumbusha umuhimu wa sekta ya kilimo, Waziri mkuu aliwaambia washiriki zaidi 1001 wakiwemo wajibika wa kilimo na ufugaji na wasimamizi wa mashirika ya kilimo na ufugaji kwamba hiyo ni taaluma inayojikingia kimaisha wanyarwanda 90%.

Katibu wa serikali katika wizara ya kilimo na ufugaji Tony Nsanganira alisema kuwa jando hilo liliundwa kwa lengo la kuboresha na kuongeza mavuno ya kilimo na ufugaji.

Waziri mkuu Anastase Murekezi aliwaomba kuendelea kufanya na bidii na kuweka nguvu zao pamoja ili wakulima wapate mazao ya kudumu kwa shabaha la kuendeleza taifa.

Alisema “ Mimi Nawaomba kushiriki katika maendeleo ya nchi yetu, mkifanya bila kusita na kuwa wa kwanza kuboresha kilimo na ufugaji, tunategemea kufanikiwa”.

Waziri Murekezi aliwaomba pia kusaidia na kutetea wale wanaowaongoza kwa lengo la kuwaendeleza na kujilinda unyang’anyaji wa kula mali za wasiojiweza.

Msaidie kuunganisha wakulima, wafugaji na wamiliki viwanda vinavyozallisha bidhaa mavuno ya kilimo na ufugaji. Nataka uaminifu uwe ngao katika mipango iliyotekelezwa na serikali kama Girinka”. Waziri mkuu aliongeza.

Shirika za serikali na wizara ya kilimo na ufugaji ziliombwa kushiriki katika utafiti unaoegemea matatizo yanaokumba wakulima na wafugaji, waziri mkuu aliwashukuru washiriki na wale waliowasaidia katika mafunzo haya na kuwakumbusha kuwa nchi inahitaji msaada wao na nguvu zao katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments