Nyamasheke : Majambazi saba wamekamatwa

Polisi ya Rwanda imetangaza kuwa imewakamata majambazi saba katika tarafa la Bushenge, Wilaya ya Nyamasheke, Magaharibi mwa Rwanda.

Polisi inasema kwamba hawa majambazi wanatuhumiwa na raia kuwategemea njiani wakachukua mizigo yao, vibeti, faranga na kwa nguvu halafu wakakimbia.

Mkuu wa Polisi wilayani humo , SP Justin Rukara alisema ‘’ nawashukuru viongozi wa vijiji kwa kushirikiana nasi , hao majambazi tuliwakamata baada ya kupewa habari na viongozi wa chini.’’

Si viongozi tu, mkuu huyo wa polisi alipongeza raia kwa kushirikiana vyema na uongozi wao na wa Polisi pia.

Aliwaomba raia wakati wowote kumuona muhalifu, wajulishe polisi ili akamatwe kabla ya kuiba au kuua watu.

Majambazi waliokamatwa ni Niyonsaba Amiel, Rukundo Joseph, Hakizimana Samuel, Harerimana Zachée, Byiringiro Olivier, Kwizera Sion, na Nsengiyumva Emmanuel, hawa wote hivi sasa wanafungiwa katika kituo cha polisi Shangi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments