Wanyarwanda wawili wametakiwa kifungo cha maisha na mahakama ya Ufaransa.

tangu kushoto Octavien Ngenzi na Tito
Wanyarwanda wawili wakiwemo Tito Barahira na Octavien Ngenzi ambao wanatuhuhumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka wa 1994 na mahakama ya Paris Nchini Ufaransa.

Wote wawili wanashitakiwa makosa ya kijinai waliotenda katika Kabarondo, mkoani Kibungo. Baada ya miezi miwili ya kusikiliza mashuhuda, Mwendesha mashitaka Philippe Courroye ametangazia shirika la AFP kwamba ni lazima watuhumiwa wafungwe maisha yao katika gereza kwani wao wanaonekana klutenda uhalifu wa mauaji ya kimbari dhidi ya watusti mwaka wa 1994 nchini Rwanda.

Octavien Ngenzi mwenye umri wa miaka 58 anatuhumiwa kutoa masharti ya kuwakata mapanga watutsi. Wakati Tito Barahira wa miaka 58 anashitakiwa kuongoza mauaji katika wilayani humo, amabako alikuwa silaha za jadi mikononi mwake.

Octavien na Tito wanatuhumiwa kuchangia mauaji alipotokea tarehe 13, Aprili, 1994 katika kanisa la kikatoliki la Kabarondo.

Philippe Courroye amekumbusha kwamba watu hawa, waliokamatwa nchini Ufaransa wamehukumiwa chini ya uwezo wa mamlaka nzima ya mahakama za Ufaransa. Kesi hii ni ya pili kushughulikiwa nchini Ufaransa kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments