Madonna afanya ziara Kenya

Madonna alikutana na mkewe rais Kenyatta bi Margaret
Mwanamuziki wa POP kutoka Marekani Madonna yuko nchini Kenya kwa ziara ya kibinafsi.

Haijulikani alitua lini ila aliwaamkua wakenya kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter

Hapo jana alikuwa ametembelea kitongoji duni cha Kibera.
Huko alipiga picha ya hali duni ya miundo mbinu katika eneo hilo nje kidogo ya jiji la Nairobi kabla ya kuchapisha picha mbili akiwa na mwanamke mmoja aliyemtaja kama mama Sofie.

Mara ya mwisho mwanamuziki huyo alipozuru Afrika alikwenda Malawi ambapo alipanga watoto David Banda na Mercy James.

Haijulikani haswa iwapo yuko nchini Kenya kwa shughuli sawa na hiyo.

Malkia huyo wa Pop anafahamika kote duniani kwa vibao vyake muruwa La Isla Bonita, Like a Virgin (1984), Like a Prayer (1989), Erotica (1992), Music (2000), American Life (2003),miongoni mwa vingine vingi.

Mwaka wa 2015, Madonna aliachilia album yenye kichwa Rebel Heart.
Madonna ana umri wa miaka 57.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments