Rais wa Uhindi amewatakia wanyarwanda siku njema ya ukombozi.

Leo tarehe 04, Jualai Wanyarwanda wanaadhimisha siku ya ukombozi kwa mara ya 22 tangu Rwanda kukomboa na waliokuwa wapiganaji wa Rwanda Patritic Front RPF kutoka mikononi ya uongozi bovu uliyotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka wa 1994.

Katika ujumbe mzito aliyompelekea Paul Kagame, Shri Pranab wa Uhindi alimuambia kwamba raia wa Uhindi wanamtakia siku njema mwenyewe na wanyarwanda kwa ujumla.

Aliendelea kusema kwamba wakati huu Rwanda inaadhimisha siku ya ukombozi kwa mara ya 22 nchi ya Uhindi inaendelea kuunga mkono Rwanda kujenga jamii ya kidemokrasia na kuboresha utoaji wa huduma za kisheria kwa kila raia.

‘’Rwanda na Uhindi wataendelea kushirikiana ili kuboresha manufaa ya wananchi.’’
Rais Uhindi Shri Pranab alihakikisha.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments