Waziri mkuu wa Israel kuzuru Rwanda.

Tangu hii leo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameanza ziara yake ambako Yeye anatarajia kutembelea nchi za Afrika Mashariki na ya kati.

Katika ajenda, Bwenjamin Netanyahu anasubiriwa nchini Uganda hii leo ambapo atatembelea mahali kakake Yonatan Netanyahu alipofariki wakati wa kuokoa wayahudi waliotekwa nyara na magaidi.

Halafu ataendelea nchini Kenya,kabla ya kuingia Rwanda jumamosi asubuhi tarehe 6, mwezi huu.

inasemekana kuwa atakuwa pamoja na viongozi wakuu na wafanyabiashara mashuhuri kutoka Israel.

Nchini Rwanda, Netanyahu atatembelea ukumbusho wa mauaji ya kimbari Rusozi/ Kigali na kukutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame. Baada ya ziara yake huku, waziri mkuu wa Israel atapanda ndege aende nchini Ethiopia.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments