Rwanda imepuuzilia mbali madai ya uuzaji wa binadamu.

Tangu kushoto, Bi. Mukantabana Mathlide
Balozi wa Rwanda nchini Marekani amepuuzilia mbali madai ya ripoti iliyotolewa na idara ya Marekani kuhusu uuzaji wa watu (Human Trafiking), ripoti hiyo inashtaki Rwanda kuhusika na uhalifu wa kuuza watu.

Kupitia tangazo rasmi lililopakiwa kwenye tovuti ya serikali ya Rwanda, Balozi Mukantabana Mathlide amekanusha hayo mashtaka, amesema kwamba Rwanda imeweka mikakati imara ya kukomesha uhalifu wa Human Trafiking ndani na katika ukanda.

Yeye alisema’’chochote hii ripoti inasema kuhusu nchi yangu ni uongo, hakuna uhusiano na ukweli hata kidogo, hii ripoti ina faida za kisiasa.’’

Aliendelea kusema hii Ripoti ni mbinu moja miongoni mwa njia zinazotumiwa na makundi yanao faida fulani kwa kuchafua Rwanda. Mathlide alisema hii ripoti inashtaki Rwanda kuingiza watoto wakimbizi katika jeshi yaani Rwanda ni nchi inayofanya iwezekanavyo kwa kubembeleza wakimbizi.

Balozi Mukantabana alisema ‘’nguvu tunazotumia kwa kupa kimbilio ndugu zetu ni miongoni mwa thamani ya wanyarwanda kuliko hizo ripoti zinazoandikiwa nje.’’

Alihitimisha akisema ‘’kutangaza hivo, ni kuchafua sifa ya Rwanda kimakusudi, Rwanda ni nchi inayotumia nguvu nyingi ili watu hususan wanawake na wasichana wawe na utulivu bila kuuzwa na kunyanyaswa kijinsia, Mimi ninapuuzilia mbali madai hayo.

Hii ripoti itwayo “Trafficking in Persons Report 2016”, inasema kwamba Rwanda ni njia inayotumiwa na wahalifu wanaouza watu na nchi yenye sifa ya kukuika haki za watot na wanawake,...

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments