Redio K.FM kufutwa kwenya masafa ya FM Rwanda.

Katika tangazo rasmi lililiotolewa na Kampuni Binafsi ya vyombo vya habari Nation Media Group(NMG) ya Kenya, NMG inasema kwamba inajiandaa kufuta kwenye masafa ya FM nchini Rwanda Redio inayomiliki itwayo K-FM inayosikika kwenye 98.7 tarehe 30, Juni, 2016.

NMG inasema kuwa itafanya hivo kwa kukuza NTV na kuifanya runinga ya kisasa inayorusha habari yenye ubora wa kisasa.

Sio K-FM Rwanda tu, NMG inasema kwamba Yeye itafunga Nation FM na Q-FM za Kenya lakini licha ya kufutwa kwenye masafa ya FM, wataendelea kurusha matangazo kwenye intaneti.

NMG ni kampuni inayomiliki vituo vya habari kama The Daily Nation, The East African, The Daily Monitor, Easy Fm, NTV, NTV Uganda, The Citizen na kadhalika.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments