Kirehe : Vijana wanatakiwa kuitokomeza itikadi ya mauaji ya Kimbari.

Katika kipindi cha kukumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi mwanzoni mwa mwezi Aprili, asilimia 90 ya waliotuhimiwa itikadi ya mauaji ya kimbari ni vijana.

Muzungu Gerald, meya wa wilaya ya Kirehe, mashariki mwa Rwanda na pia mwakilishi wa Chama cha RPF wilayani humo, katika mkutano wa wanachama Gerald alikimbusha vijana kwamba wao ni njia rahisi ya kuambukiza itikadi ya mauaji ya kimbari, hivyo wao wanapaswa kuwa kwenye mstari wa mbele kwa kukabiliana na hiyo maradhi ya itikadi.

Gerald alisema “tunaweka nguvu zaidi katika tume vijana wanachama wa RPF-Inkotanyi, tunazo kanuni za kuitokomeza itikadi ya mauaji ya kimbari na ubaguzi wa kikabila, na pia tumeshapata msimamo kuhusu kosa hilo la kijinai nchini Rwanda.’’

Kuhusu chama, Muzungu alisema kwamba mwaka huu RPF walifanikiwa kuliko mwaka jana.

Katika mkutano tarafa la Nyarubuye,Kigarama na Kigina walipewa tuzo kama watu waliokuja mbele kwa kupa msaada na kusindikiza chama.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments