TP Mazembe yainyuka Yanga

Tarehe June 28 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilirejea katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ndio uwanja inaoutumia kama uwanja wake wa nyumbani kucheza mechi yake ya pili hatua ya nane bora dhidi ya klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Moyo wa kila mshabiki wa timu hii hujaza huzuni ambayo hawezi kusahau kamwe.

Katika mchezo huo wa Kundi A lenye timu za Medeama ya Ghana, Mo Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya Kongo na Yanga, umemalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo limefungwa dakika ya 74 na Merveille Bope, TP Mazembe walionekana kucheza kwa umakini na uzoefu mkubwa, kitu ambacho kimeisaidia kupata alama tatu.

Goli la Mazembe lilitokana na mpira wa adhabu ndogo baada ya Kelvin Yondani kumuangusha Thomas Ulimwengu nje kidogo ya eneo la hatari. Mpira wa adhabu ndogo ulimfikia Merveille Bope na kuupachika kambani baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuuondosha kwenye eneo lao la hatari.

Tayari Yanga imeshacheza mechi mbili kwenye hatua ya makundi, wamefungwa zote kwa goli moja (kila mechi) huku wao wakiwa bado hawajafunga bao hata moja katika mechi walizocheza.


Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments